Header Ads

]

Fahamu hasara za matumizi ya P2 katika afya ya Uzazi#


P2Vidonge hivi vya p2 vimeshika umaarufu Sana kwakipindi hiki ,Siku za hivi karibuni: wadada wengi imekua Kama desturi yao. Wanakula dawa Kama njigu vile daah:

P2 ni kifupi na Postinor-2, ni dawa inayotumika kwa dharula tu. Vidonge vya P2 havitakiwi kutumika kama njia ya mara kwa mara kuzuia mimba.

Vidonge vya p2 vinatakiwa kutumika tu endapo njia zingine za kuzuia mimba zimefeli. Kwa mfano kondomu kupasuka katikati ya tendo au umefanya tendo na kusahau kuvaa kinga na upo kwenye siku za hatari.

Vidonge vya P2 vinafanya kazi kwa kuzuia yai kupevuka wakati wa mzunguko wa hedhi. Pia P2 inafanya uteute wa ukeni kuwa mzito sana na kufanya mbegu kushindwa kuogelea kwenda kwenye yai. Kazi ingine ya P2 ni kubadili ukuta wa mji wa mimba ili kuzuia mimba kujishikiza.

Ufanisi wa Vidonge vua P2
Vidonge vya P2 viazuia kushika mimba endapo vitatumika ndani ya masaa 72 baada ya kufanya tendo bila kinga. Inakadiriwa kwamba P2 ina ufanisi karibu asilimia 85 kuzuia mimba. Endapo vidonge vitatumika ndani ya masaa 24 baada ya kufanya tendo, ufanisi unaongezeka zaidi ya asilimia 95. Ufanisi utazidi kupungua kadiri masaa yanavyosogea

Kutumia vidonge vya P2 hvitasaidia kama tayari una mimba na pia havikuzuii kupata magonjwa ya zinaa kama ukimwi, kisonono na chlamydia.

Dawa hii inaweza isifanye kazi vizuri kwa baadhi ya wanawake hasa wenye uzito mkubwa mfano uzito zaidi ya kilo 74 na kama upo kwenye dozi ingine ya dawa. Zungumza na daktari wako kama dawa itakufaa kulingana na afa yako.

No comments

Dr Mgasa Mhoja. Powered by Blogger.