Header Ads

]

JE WAJUA PRIAPISM NI NINI? Jua ukweli kuhusu priapism na matibabu yake.


karibu kwenye gammaL0VE leo tunakjuza hii PRIAPISM,  Priapism ni jina la kitaalam ikimaanisha ni hali ya UUME (penis) kusimama  kwa masaa bila ya viamshi vya hisia (kiraruraru) au baada ya viamshi (vichocheo)vya hisia kuacha. 

Natumaini nimeanza kueleweka japo bado ujajua inakuaje uume uendelee kusimama wakati hakuna hisia, hii itakusaidi kuelewa 
kwakawaida ili uume usimame basi unahitaji mzunguo wa damu mzuri ukiambatana nahisia zilizochochewa na mifumo ya fahamu, kwa kawaida mfumo wa parasympathetic ndio huusika katika swala lakusimama kwa uume, baada ya   kusimama ndipo mfumo wa sympathetic huingia nakusababisha mtu kupizi(kukojoa)  ndipo mfumo wa awali husimama ndipo damu hupungua kwenye uume  nakuruhusu uume kusinyaa (kulala)  inaposhindikana kwa damu kupungia kwenye uume ndipo swala hili la priapism hutokea.

 yani hali hii ina aina tatu yani PRIAPISM 1, Ischemic (mtiririko wa chini)  2. non ischemic (mtiririko wa juu)  3.recurent ishemic (yakujirudiarudia)

 Naomba ifahamike kwamba aina ya kwanza  ischemic priapisim  ni naambatana na maumivu ya uume hii hutokana kwamba damu inashinda KUTOKA kwenye uume na kusababisha uume kuendelea kusimama, hii ikizidi msaa manne tu huchukuliwa kua ni jambo la dharula.


VITU VINAVYO WEZA KUCHANGIA PRIAPISM
1. ugonjwa wa Sickle cell
2.kansa ya damu
3.Matumizi mabaya ya dawa katika matibabu kwamfano trazodone, thorazine dawa za kutibu magonjwa ya akili,
4. Madawa ya kulevya yakiwemo marijuana, cocaine,
5. Jeraha ; jereha la mshipa wa damu (ateri ya uume)  huweza kuzuia mzunguko wa damu wakawaida hivyo kusababisha damu kuzidi baki kwenye uume.


MADHARA YA TATIZO HILI LA PRIAPISM
 nimuhimu kwa mtu ambae uumewake umezidi kusimama bila kulala kwa zaidi ya masaa manne kutafuta msaada w matibabu, ifahamike kua damu iliojaa kwenye uume haina oxygen yakutosha  hivyo basi tissue za uume huitaji oxygen sasa basi tisue zinaweza kuharibika kutokana na tatizo hilo.
kuharibika kwa tissue kunaweza anza baada ya masaa 4-6 (manne hadi sita)

Bila ya matibabu ya haraka, kuharibika kwa neva kunaweza kutokea hivyo kuchangia katika matatizo ya kusimamisha uume. ifahamike tisue zinazo husika na hisia katika uume zikifa haziwezi kurejeshwa vema.


MATIBABU (MAMBO YA KUFANYA PRIAPISM IKIKUTOKEA)
kama ambavyo gammaLOVE tumetangukia kukueleza aina za PRIAPISM vivyohivyo hata matibabu yake hutnemeaaina hizo.
kama auume umezidi kusimama ikiw\ kabla ya masaa manne (4)  hatua za kitabibu za kupunguza damu kwenye uume kwa dawa zaweza fanyika na kusaidia uume kulala. kama ni masaa (4-6)  matibabu huwa ni rahisi, ikiwa ni zaidi ya masaa 6 matibabu kwa dawa husindikana hivyo hupelekea njia zifuatazo  kutumika.
 1. kuweka mabonge ya barafu kwenye eneo la uume, hii hupunguza uvimbe na damu kujaa
2. ASPIRATION ; hili niina la kilaam la procedure ambayo huifanya daktari ili kufonza damuilio jikusanya kwenye uume hii hupunguza maumivu kwa haraka.
3. UPASUAJI; kama njia ya ASPIRATION na KUTUMIA MAMBONGE YA BARAFU  IMESHINDIKANA  upasuaji husaidia kurudisha mfumo wa mzunguko  wa damu kawaida, ikiwa nikutoa damu yote ilio jikusanya nakuganda kwenye uume.

 NATUMAINI UMEJIFUNZA NAKUELEWA ( usiavhe kutoa maoni yako ili kuboresha huduma ya gammaLOVE) Usisite kushare ili nawngine wahahamu


(c)gammaLOVE THE LOVE OF HUMANITY





No comments

Dr Mgasa Mhoja. Powered by Blogger.