Header Ads

]

FAHAMU UHUSIANO KATI YA MLO NA AFYA YAKO. ( Usichukulie poa unakula ili uishi au unaishi ili ule?)

Karibu katika gammaLOVE, leo mambo ni moto usichukulie poa, tutazungumzia mlo na afya jinsi vinavyo oana. yanii waswahili husema kua nikama pande mbili za sarafu huwezi kuvitenganisha.  Ushawahi jiuliza unaishi ili ule au unakula ili uishi? 

Mlo  ni mkusanyiko wa vyakula mbalimbali ambavyo kwa pamoja huimarisha na kuujenga mwili wa binadamu na wanyama kwa sababu vinaleta virutubishi vyote vinavyohitajika.
Afya ni hali ya kujisikia vizuri kimwili, kiakili, kiroho na kiutu bila kusumbuliwa na ugonjwa wowote.

Afya ya binadamu itakuwa njema kama atafuatilia kanuni na taratibu bora za afya. Hiyo inajumuisha mlo kamili, yaani chakula chenye virutubishivyote, vikiwemo protini, wanga na mafuta (hiyo iwe katika asilimia ndogo sana).  vivyo hivyo mpenzi na mfuatiliaji wa gammaLOVE maradhi nikinyume cha afya

Ugonjwa
 (pia maradhi) ni hali ya mvurugo katika utendaji wa kawaida wa shughuli za mwili na roho inayoathiri vibaya stareheya kiumbehai. Hakuna tofauti kamili baina ya ugonjwa na hali ya kujisikia vibaya.

napenda kuku fahamisha hili kama ulikua hujui kua kunauhusiano mkubwa sana juu ya afya yako na mfumo wa milo yako. pengine umekua ukichukulia poa juu ya milo yako, wakat mwingine umekua ukisema kikubwa uhai, unakula ili uishitu. mmh yaweza ikawa ni sawa kwa fikra za kawaida lakini uhalisia ni kwamba mlo mbovu ukupelekea maradhi na mlo mzuri hukupelekea afya.
gammaLOVE haiishii hapotu, ukipatwa maradhi kipi kinafatia? 
je  ushawahi jua kua maradhi nayo yanaweza sababisha na kuathiri mlo wako?  jibu ni ndio,  kwa hiyo vitu hivi maradhi na milo mbovu huelekeana (kila mmoja humsababisha mwenzake).


JINSI MARADHI YANAVYO WEZA KUATHIRI MFUMO WA ULAJI WAKO (MLO)

Nakusisitizia maradhi yote haijalishi yako kwa uzitokiasi gani hupunguza ulaji wako.(kukosa hamu ya kula)
maradhi husababisha kupotea kwa virutubisho mbalimbali vya mwili, ikiwa katika njia namifumo mbalimbali mfano 
1.kuzuia kuchukuliwa kwa virutubisho baada ya mmeng'enyo (absoption)
2.Hupotezavirutubisho mojakwamoja kutoka mwilini 
3. Huathiri mfumo wa utendajikazi kwa kikemilali mwilini (metabolic responce)
mbali na mfumo wa mwili kuathiriwa maradhi huathisi kwaupande mwingine mfumo wa ulaji wako japo sio ojakwamoja, kwa mfano hupunguza uwezo wautendaji kazi,hupunguza uzalishaji hivyo basi mtu hufikia hali yakukosa mlo mzuri.

ATHARI ZA MLO DHIDI YA MARADHI
kiulahilisa utapiamlo niswala laupungufu wa virutubisho mwilini,  kukosefu wa virutubisho kamavyote hivi vinavyo stahili upelekea yafuatayo 
1.Hupunguza uwezo wa kinga kushambulia vimelea vya magonjwa.
2. Hupunguza kinga dhidi ya sumu za bacteria
3. Hupunguza uwezekano wa kidonda kupona haraka
kabla sijamaliza  napenda nikupe mfano wa magojwa ambayo huathiri virutubisho na mlo kwa ujumla.
kuhara- husababisha malabsoption na hali ya kukosa hamu ya kula
Magonjwa ya mfumo wa hewa hupunguza hamu ya kula
surua hupunguza vitamini A, huleta homa, huathiri hata misuli ya mwili,

Malaria husababisha upotevu wa vitamini A na Zink mwishoe hata husababisha anemia na ukuaji hafifu wa mtoto(kudumaa)


gammaLOVE tunashauli uzingatie shauri za milo ili ujikinge na maradhi, na jikinge na maradhi lili usiathiri mfumo wako wa mlo.



No comments

Dr Mgasa Mhoja. Powered by Blogger.