Header Ads

]

Fahamu Dalili za mwanamke akiwa Mwezini (kwenye siku zake) PATA KUJUA ITAKUSAIDIA

   Habari wapenzi WA gammaLOVE

 
     Ili kuhakikisha unapata kitu sahihi  kwaajili ya afya yako Leo tunakuletea hili Kuhusu afya  kwa wanawake kuingia mwezini (kwenye siku special kwaajili yao) . Sijui nikotokana na mazoea mabovu  watu huogopa kujulikana Kwambali wapo kwenye sikuzao wakihisi ni swala LA aibu. Sio kweli.. Nivema nijambo la kawaida sana kwa wanawake. 

     Sio Lazima awe mwanamke tu kujua mwanamke mwenzake kaingia kwenye siku zake.  Hata Wewe mwanaume inakupasa kujua. Unaweza ukawa baba  au mume  unajua nijinsi gani ya ku msaidia wakalibu yako. Kwa baadhi ya watu hua wanakumbwa na matatizo makubwa kuzimia hata kupoteza damu Nyingi.. Unashauliwa ujue mtuwako wa karibu Kama anapatwa Na matatizo haya uweze kumnusuru na kuokoa maishayake. 

      zifuatazo ni dalili za mwanamke akiwa mwezini 
Kuongezeka kwa ukubwa wa  matiti:Katika kipindi hiki mwanamke anaweza kuona matiti yake yameongezeka ukubwa na muda mwingine kulazimika kubadili sidiria(bra).



Kupata chunusi(acnes):Mabadiliko ya viwango wa homoni mwilini husababisha ngozi kuzalisha kiwango fulani cha mafuta na kuonekana kama chunusi.Mara nyingi chunusi hizi zinauma hasa mtu anapojaribu kuzifinya



Tumbokuuma(abdominal cramps):hutokana na maandalizi ya ukuta wa mji wa uzazi(uterine walls) kubomoka au kumong’onyoka.Kupunguza maumivu ya tumbo lipapase tumbo(massage) na pia hakikisha utulivu(relaxation),basi tumbo litapoa kabla ya nusu saa kuisha.
Kukosa hisia za kufanya jambo(moodiness):Hii ni kati ya dalili kubwa zaidi iliyowapata wanawake waliokuwa wengi ktk kipindi hicho kuelekea siku zake za hedhi.Hii hutokana na kiwango cha kichochezi(hormone) kiitwachoEstrogen kuongezeka mwilini ,kibaya zaidi ni kuwa hali hii huweza kuathiri mfumo wa maamuzi(judgement).


Matiti kuuma yanapoguswa(breast tenderness):Hali hii wanawake wengi huishuhudia pale wanapojaribu kuvaa sidiria(bra) zao japo wanaweza wasihisi hali hiyo wanapojigusa au kujipapasa  kwa mikono yao.Hii hutokana na kuongezeka kwa kiwango cha homoni iitwayoprogesterone ambayo husababisha maeneo ya titi kuwa rahisi kuhisi(sensitive).


Kuwa na hamu ya kula sana(food cravings):Hali hii hutokea kabla na wakati wa hedhi,hii hutokana na kupungua kwa kiwango cha homoni ziitwazoSerotoninnacortisol.


Msongo wamawazo(depression):Katika kipindi hiki mwanamke anakuwa na tatizo la msongo wa mawazo sana na kumpelekea kuwa mambo mabaya mabaya ikiwemo kumdhuru mtu au kujidhuru yeye mwenyewe.Hali hii husababishwa na kupungua kwa homoni zinazohusika na msukumo wa kifikra(emotions) kupungu a kutokana na kuongezeka kwa homoni zaestrogen na progesterone.Kupunguza tatzo hili unashauriwa kutumia chakula chenye kiwango kizuri cha protini mfano;mayai na samaki.

Kichwa kuuma(migraines):Aina hii ya kuuma kwa kichwa huwa ni maumivu ya kuvuta/kupwita(throbbing pain) ambacho kinaambatana na kupata kichefuchefu na kupoteza uoni(vision).Tatizo hili inaweza kutibiwa kwa dawa za kupunguza maumivu(pain killers),kula matunda na kunywa maji ya kutosha.


Tumbo kujaa gesi(bloating:Tatizo hili linaweza kutibiwa kwa kumpa mgonjwa kiasi sitahili cha madini ya Kalsiamu(calcium)na magnesiamu(Magnessium).


Kua makini usichukulie kua period nikutu change kawaida  kila mwezi  mabadiliko hutokea..
Wengine hupoteza damu Nyingi..
Huenda mwezini kwasiku Nyingi Zaidi  nikiweza kisababisha madhara.
(gammaLOVE)

No comments

Dr Mgasa Mhoja. Powered by Blogger.