Header Ads

]

Unazijua njia 5 za kukuzuia kukoroma usingizini?



THE LOVE OF HUMANITY 


welcome to gammaLOVE yawezekana imekua kero sana hasa ukiwa umelala namtu anae koroma, wengine wamekua wakikosa usingizi kabisa kutokana na kero  zakukoroma. 

hua unajisikiaje endapo umelala na mpenzi wako anakoroma halafu wewe hukoromi?

leo nakusaidia kulisolve tatizo hilo.
1. Kuzingatia uzito na mlo bora. Kuwa na uzito mkubwa(unene) huweza kusababisha kukoroma. Mafuta yaliyozunguka shingo hupunguza njia ya hewa na kuzuia hewa kupita kiurahisi kutoka nje au kuingia ndani.
2. Jaribu kulala kwa ubavu badala ya kulala kwa mgongo. Wakati wa kulala kwa mgongo, ulimi wako au tishu yoyote ya mafuta huweza kulalia ama kukandamiza na kuziba njia ya hewa. Kulala kwa ubavu huzuia hii.
3. Usinywe pombe kabla ya kwenda kulala. Pombe hufanya misuli yako kupumzika zaidi kuliko kawaida wakati wa usingizi.
4. Acha kuvuta au punguza uvutaji wa sigara. Moshi wa sigara huathiri njia ya hewa katika pua na koo, na husababisha uvimbe. Hii husababisha kupungua kwa njia ya hewa na kusababisha kukoroma.
5. Hakikisha pua zako zipo wazi. Ni vizuri upumulie pua yako badala ya mdomo wako. Ikiwa kuna vikwazo vinazuia pua yako ni vizuri kumuona daktari wako, huweza ukawa na allergy au matatizo mengine yanayo jirudia mara kwa mara kama mafua vinjama vya puani(nasal polyps).
Tupe support yako kwa kulike page zetu

No comments

Dr Mgasa Mhoja. Powered by Blogger.