Header Ads

]

Je, wajua pilipili husaidia katika kuimarisha nguvu za kiume? pata kujua na vyakula vingine

Ndugu mfatiliaji wa karibu wa gammaLOVE, leo tunakuletea kuhusu pilipili,je wajua pilipili huongeza nguvu za kiume? natumai jibu ndi ndio au hapana. pengine pilipili umekua ukiitumia kama appetizer tu, katika huongeza hamu na radha yachakula. Zipo pilipili za kuwasha kama pilipili mbuzi na pilipili kichaa lakini pia zipo ambazo haziwashi kama pilipili hoho, leo nitaonngelea zile pilipili zinazo washa.

kabla ya kuendelea nahii jinsi zinavyo imarisha nguvu za kiu
me kwanza napenda nikukumbushe faida za kawaida za pilipili, zinanzo washa

Ina kiiasi kikubwa cha vitamin c.   husaidia kupunguza uzito; pilipili huongeza kasi ya mwili kufanya kazi na kuchoma mafuta[metabolism],

hutunza macho; lutein ni enzyme inayopatikana kwenye pilipili, katika umri mkubwa wa maisha hufanya kazi ya kuzuia kutokea kwa mtoto wa jicho,huu ni weupe unaotokea kwenye lens ya jicho na kumfanya mtu apate upofu.

hupunguza kasi ya uzee; kiasi kikubwa cha vitamin e kilichopo kwenye pilipili hulainisha ngozi sana na kumfanya mtumiaji kuonekana kijana na mwenye nguvu hata katika umri mkubwa wa maisha.

husaidia mmeng'enyo wa chakula; pilipili husaida mwili kutengeneza kiasi kikubwa cha kemikali ya hydrochloric acid inayopatikana tumboni ambayo kazi yake ni kuongeza mmeng'enyo wa chakula hivyo kuupa mwili virutubisho vyote muhimu. pia kwa lugha ya kitaalamu husema huongeza GIT motility.


JINSI PILIPILI INAVYO IMARISHA NGUVU ZA KIUME
 Nguvu zakiume hutegemea sana hisia, na mzunguko mkubwa wa damu, hivyo basi pilipili huhusika kuufanya mzunguko wa damu uwe mzuri, system inayo control nguvu zakiume kwa lugha ya kitaalamu huitwa parasympathetic system hivyo basi pilipili huusika mojakwamoja katika kuchochea parasympathetic system ndopo sasa mtiririko wa damu hua mzuri nakuweza damu nyingi kufika kwenye uume, hapo ndipo uume unaweza kusimama vizuri.

sio pilipili pekeyake inayo imarisha nguvu hizi vipo na vyakula vingine vinavyo weza kuimarisha nguvu za kiume kama vifuatavyo.


1.karanga
Karanga ni chanzo kikubwa cha kujenga protini mwilini. Karanga huwa na kiwango kikubwa cha amino asidi ambayo husaidia kuweka vizuri mfumo wa damu, 

2..MVINYO MWEKUNDU
Mvivyo mwenyekundu unatajwa kuwa na uwezo wa kuuchangamsha mwili na kuongeza msukumo wa damu, kiasi cha kumuondolea mtu uchovu kabla na baada ya tendo la ndoa, hivyo ni muhimu kunywewa hasa na wale ambao wanasumbuliwa na tatizo la kushindwa kurudia tendo. (kumbuka nikiwango kidogo nasio kuzidisha ukizidisha kuwa kinyume)

3.Ndizi 
Wakati unafikiria uwezo wa kufanya vema tendo la ndoa unatakiwa kuwaza juu ya uimara wa misuli ya mwili ambayo inatajwa kuwa ni sehemu kuu na yenye muhimu katika kujamiiana. Kwa msingi huo ulaji wa ndizi mbivu unatajwa kusaidia kujenga misuli mwilini na kumfanya mtu aweze kuwa hodari katika tendo la ndoa.

4.Pweza 
Aina hizi za samaki zinazovuliwa baharini huwa na madini ya zink na chumvi ambayo yanatajwa kusaidia uzalisha wa vichocheo vinavyohamasisha msisimko wa mwili wakati wa tendo la ndoa.

5.Chocolate
Chocolate inasaidia kuongeza stamina kwenye kufanya mapenzi kwasababu ina viambato vya phenylethylamine na alkaloid. Phenylethylamine ni kiambato kinachopelekea kujisikia vizuri, hasa wakati wa kufanya mapenzi na alkaloid huongeza stamina na nguvu wakati wa mapenzi.

6.Parachichi
chakula ambacho husaidia kuongeza uwezo wa mtu kufanya tendo la ndoa ni Parachichi. Tunda hili linauwezo mkubwa wa kuzalisha vitamini E ambayo husaidia katika uzalishaji wa homoni. Inatajwa kuwa watu wanaotumia tunda hili kwa wingi huwana msisimko mkali wa kimapenzi na kwa upande wa wanawake husaidia kuongezamajimaji yenye utelezisehemu za siri na hivyo kuzuia uwezekano wa kuchubuka wakati wa kujamiiana.

7. Vitunguu swaumu
Kitunguu saumu kina allicin, kiambato kinachosaidia mzunguko mzuri wa damu kwenye viungo vya uzazi. Kuwa na mzunguko mzuri wa damu kwenye uume ni sababu kubwa ya kuongeza stamina ya kufanya mapenzi.

8.Tikiti maji 
matikiti maji ni tunda muhimu sanna kwa kulinda ndoa inatakiwa walau kwa siku upate vipande viwili au vitatu na sasa yapo kwa wingi ushindwe wewe na ni muhimu ukala na mbegu zake.

9.Maji
ni muhimu pia kwa kukuza uume na inashauriwa kunywa lita tano na zaid japo sio vyema kukaa na mkojo muda mrefu. maji pia usaidia kuondoa ugonjwa mwilini na homa za mara kwa mara.tikiti majihusaidia kuamasha hamasa mwili.Mwisho wa aina hizi za vyakula ni TIKITI MAJI ambalo linatajwa kuwa na virutubisho vingi vyenye uwezo wa kuusaidia mwili kuwa na nguvu za kutosha kufanya tendo la ndoa.

10. Promegranate
Ni aina fulani ya matundamekundu yanayofananana na apple. Haya yatajwa kusaidia kuamsha mishipa ya fahamu na kuweka mawasiliano sahihi ya mwili na hivyo kumuongezea mtu uwezo kwa kufanya tendo la ndoa kwa hamasa kubwa.

pamoja nakujua sababu za kuongezeka kwa nguvu za kiume ni vema ujue na sababu za kupunguza nguvu hizo ili uweze kujizuia na kufanya afya yako iwe bora maradufu.




Sababu za kukosa nguvu za kiume, upungukiwa protini na hivyo kukosa amino asidi mwilini,kula vyakula vya mafuta,magonjwa ya muda mrefu,magonjwa ya kisukari na pressure,pombe kupita kiasi na sigara,uchafu wa mwanamke au mahali linapotendeeka tendo kwa mfano hewa safi,kukosa muda wakuupumzika yaanii kufanya kazi sana na kuwa na muda mchache wakulaa, kuwa na msongo wa mawazo, Kutokuwa na mzunguko mzuri wa damu mwilini, hasa sehemu za viungo vya uzazi kwa mwanaume.,Kutokuwa na kiwango cha kutosha cha homoni ya Testosterone




 gammalove the love of humanity
(2018)




No comments

Dr Mgasa Mhoja. Powered by Blogger.