Header Ads

]

Tiba ya vidonda vya tumbo na jinsi stress zinavyo sababisha tatizo hili.( ULCERS)

Ndugu mpenzi wa gammaLOVE leo utapata kujua tiba ya vidonda vya tumbo,najinsi stress zinavyo sababisha, pengine ushakutana na mapokeo mengi kuhusu sababu za vidonda vya tumbo, nawengi kutoa sababu zao leo nakupa jibu sahihi na sababu za msingi zinazoweza sababisha madonda ya tumbo. kabla hatuja fika kwenye tiba nianze nahili kuhusu stress

Stres (msongo wa ma wazo) nisababu ya vidonda vya tumbo, hii nikutokana na kwamba stress huchochea neva ya vagus (vagus nerve stimulation) 
ambayo hupelekea kuamsha hisia katika seli za pariental (pariental cell), seli hizi zikiamshwa hisia hupelekea enzem inayo itwa pepsin kuzalishwa kwa wingi pamoja na (gastric secretion) nazo huongezeka tumboni hii hupelekea kuongezeka kwa kiwango cha asidi, asidi hii humomonyoa kuta za tumbo (mucosal layer) ndipo sasa vidonda hutokea kwenye kuta hizo za tumbo.



Wakati shida ya maisha ya muda mrefu iliaminika kuwa ndiyo sababu kuu ya vidonda, hii sio tena.  Hata hivyo, bado kunaaminika kuwa na jukumu.  Hii inaweza kuwa kwa kuongeza hatari kwa wale walio na sababu nyingine kama vile H. pylori au matumizi ya NSAID.
   sio stress pekee inayo weza sababisha vidonda vya tumbo yafuatayo husababisha.
1. kuzalishwa kwa asidi nyingi katika tumbo
2. bacteria H.PYLORI
3. Dawa za kutuliza maumivu (NSAIDs)
Sababu nyingine kuu ni matumizi ya NSAIDs, kama vile ibuprofen na aspirini.  Mucosa ya tumbo inajitetea kutoka kwa asidi ya tumbo na safu ya kamasi, ambayo secretion yake inakabiliwa na prostaglandini fulani. NSAID kuzuia kazi ya cyclooxygenase 1 (COX-1), ambayo ni muhimu kwa ajili ya uzalishaji wa prostaglandini hizi. COX-2 kuchagua anti-inflammatories (kama vile celecoxib au tangu rofecoxib iliyoondolewa) inakusudia kuzuia COX-2, ambayo haifai sana katika mucosa ya tumbo, na kupunguza kiasi cha hatari ya ulinzi wa tumbo la NSAID.

Takwimbu zinaonesha kwamba watu wenye group la damu A huathirika sana na vidonda kwenye tumbo (gastric ulcers). na wale wenye blood group O huathiriwa sana na vidonda kwenye deudenam (deudenal ulcers)

AINA ZA VIDOBDA VYA TUMBO NA VIASHILIA VYAKE. ulcers
Kuna aina kuu mbili za vidonda hivi kulingana na maeneo vinapotokea 1.duodenal ulcers 2.gastric ulcers
vidonda katika duodenam (Duodenal Ulcers DU) katika hili maumivu hutokea mtu anapokua hajapata chakula, Asidi ya HCL huongezeka, uzito huongezeka, kutapika ni dadra kwa mtu huyu.


vidonda vya kwenye gastric (gastric ulcers)  katika hivi vidibda maumivu hutokea pale tu baada ya kula.uziti wa mgonjwa hupungua, kutapika ni dalili mojawapo, damu kuvuja (blood hemorrhage) hutokea kwa wingi hadi husababiha mtu kua na haja nyeusi (blak stool)


MATIBABU YA VIDONDA VYA TUMBO
Hapa katika matibabu ndio lengo letu kuu kukufikisha, naukifata dozi vizuri hakika unapona kabisa.

Dawa inayo zuia kuzalishwa kwa asidi  PROTON PUMB INHIBITOR  hii husaidia kupunguza kiwango cha asidi katika tumbo (hiii ikitumika pekeyake haitoshi kukuponesha)

TRIPLE THERAPY
Wakati maambukizi ya H. pylori , matibabu ya ufanisi zaidi ni mchanganyiko wa antibiotics 2 (. clarithromycin, amoxicillin, tetracycline, metronidazole) na kizuizi cha proton-pampu (PPI), . Katika kesi ngumu, sugu ya matibabu, antibiotics 3 (kama. amoxicillin + clarithromycin + metronidazole) inaweza kutumika pamoja na PPI . Tiba ya kwanza ya ufanisi kwa ajili ya kesi zisizo ngumu itakuwa amoxicillin + metronidazole + pantoprazole (PPI).

UpasuajiThibitisha (vagotomy)
huu upasuaji huusisha neva ya vagas.


MADHARA YA VIDONDA VYA TUMBO
Vidinda vya tumbo husababisha cancer, upotevu wa damu, anaemia, peritoneal  perforation

NATUMAI HII IMEKUSAIDIA kama unamaoni usisite kucoment kwaajili ya maboresho zaidi ya machapisho yangu.

(c) gammaLOVE 2018


No comments

Dr Mgasa Mhoja. Powered by Blogger.